UNHCR yataka uchunguzi ufanyike kuhusu machafuko ya Kinshasa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i16231-unhcr_yataka_uchunguzi_ufanyike_kuhusu_machafuko_ya_kinshasa
Umoja wa Mataifa umetaka kufanyike uchunguzi kuhusu ghasia na machafuko yaliyotokea hivi karibuni huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 28, 2016 03:45 UTC
  • UNHCR yataka uchunguzi ufanyike kuhusu machafuko ya Kinshasa

Umoja wa Mataifa umetaka kufanyike uchunguzi kuhusu ghasia na machafuko yaliyotokea hivi karibuni huko Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Kate Gilmore Naibu Kamishna Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR amesema akiwa mjini Geneva Uswisi kuwa kuna udharura wa kufanyika uchunguzi huru, wa wazi na wenye itibari kuhusu ghasia za hivi karibuni zilizotokea Kinshasa mji mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Amesema uchunguzi huo unapasa kufanyika ili kuzuia mgogoro kati ya serikali na wapinzani wa Kongo kuwa mkubwa zaidi.  

Maandamano ya wapinzani Kinshasa yaliyoibua machafuko na kusabaisha raia wengi kupoteza maisha 

Polisi ya Kongo imedai kuwa watu wasiopungua 32 wameuawa katika ghasia za wapinzani zilizotokea Jumatatu na Jumanne wiki iliyopita, hata hivyo chama cha upinzani cha Umoja Kwa Ajili ya Demokrasia (UDPS) kimesema kuwa watu100 wameuawa katika ghasia hizo.  Naibu Kamishna Mkuu wa UNHCR amesema kuwa raia 49 na polisi wanne wameuawa katika ghasia za hivi majuzi huko Kinshasa, na watu wengine 127 wamejeruhiwa. Ikiwa imesalia miezi mitatu hadi kumalizika muhula wa urais wa Rais Joseph Kabila, wapinzani huko Kongo wanasisitiza kuondoka madarakani rais huyo. 

Raia Joseph Kabila ambaye wapinzani wanamtaka ang'atuke madarakani muda wake ukimalizika