Jeshi la Libya lasonga mbele Sirte, magaidi wa Daesh waendelea kupigwa
Jeshi la Libya linaloiunga mkono serikali ya umoja wa kitaifa limesonga mbele zaidi katika mji wa Sirte unaotambuliwa kuwa ngome kuu ya kundi la kigaidi la Daesh nchini humo.
Ripoti zinasema, baada ya mashambulizi ya anga na nchi kavu ya wiki kadhaa sasa, jeshi la Libya hatimaye limepiga hatua kubwa na kusonga mbele katika mji wa Sirte ulioko kaskazini mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo sasa linawazingira wapiganaji wa kundi la Daesh katika mji wa Sirte na ngome zao nyingi zinaendelea kushambuliwa vikali.
Operesheni ya sasa ya jeshi la Libya inafanyika kwa shabaha ya kukomboa eneo la ukanda wa bahari la al Giza.
Mji wa Sirte ndio wa mwisho unaoendelea kushikiliwa na wapiganaji wa kundi la kigaidi la Daesh. Kundi hilo limeharibu kabisa sehemu kubwa ya huo.