Africa Intelligence: Serikali ya Uganda imeshadidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i19357-africa_intelligence_serikali_ya_uganda_imeshadidisha_ukandamizaji_dhidi_ya_wapinzani
Vitendo vya ukandamizaji vinavyofanywa na serikali ya Uganda dhidi ya wapinzani wa kisiasa, vimekosolewa na taasisi ya kiusalama ya Africa Intelligence nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 13, 2016 01:10 UTC
  • Africa Intelligence: Serikali ya Uganda imeshadidisha ukandamizaji dhidi ya wapinzani

Vitendo vya ukandamizaji vinavyofanywa na serikali ya Uganda dhidi ya wapinzani wa kisiasa, vimekosolewa na taasisi ya kiusalama ya Africa Intelligence nchini humo.

Taarifa iliyotolewa na taasisi hiyo imetangaza kuwa, kwa amri ya moja kwa moja ya Rais Museven wa nchi hiyo upinzani na uwekaji vizuizi wowote katika njia ya serikali, lazima ukabiliwe vikali na nguvu ya dola. Kufuatia hali hiyo, Kizza Besigye, kiongozi mkuu wa upinzani ambaye ametangaza kutoitambua serikali ya sasa ya nchi hiyo, ametaka kuendelezwa maandamano ili kufikiwa kikamilifu malengo yote.

Kizza Besigye, kiongozi wa upinzani nchini Uganda

Hivi sasa Besigye anakabiliwa na kesi ya uhaini huku vyombo vya mahakama vya nchi hiyo vikiwa vimemzuia mwanasiasa huyo kutoka nchini. Katika fremu hiyo, polisi ya nchi hiyo ilimtia nguvuni Kizza Besigye katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe wakati alipokuwa akijaribu kwenda nje ya nchi. Mgogoro wa kisiasa ulioibuka kufuatia matokeo ya uchaguzi wa tarehe 18 Februari mwaka huu, umeibua pia mpasuko wa kijamii ndani ya taifa hilo mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mmoja wa wapinzani akiwa mikononi mwa askari polisi wa Uganda

Kukosekana uwazi katika sheria, hatua ya serikali ya kupuuza matakwa ya kisiasa ya vyama vya upinzani na uchakachuaji katika chaguzi, ni sehemu ya malalamiko ya wananchi wa Uganda dhidi ya serikali ya Kpampala.