Dec 28, 2016 07:41 UTC
  • Watunisia wakataa fikra za Kiwahabi

Wananchi wa Tunisia hususan tabala la wasomi na wanafikra wa nchi hiyo wamekataa kupokea fikra za kiwahabi licha ya Saudi Arabia kutumia fedha na wakati mwingi kueneza na kusambaza fikra na mitazamo ya kisalafi na kiwahabi katia nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Mkurugenzi wa Habari wa Ofisi Waziri Mkuu wa Tunisia, Ghofran al Hussainani amesema kuwa, fikra za kiwahabi ziliingia taratibu katika anga ya elimu na vyuo vikuu vya nchi hiyo kwa uwekezaji na fedha za Saudi Arabia lakini kamwe hazikukaribishwa na kupokewa na wasomi. 

Tunisia ni miongoni mwa nchi ambako Saudi Arabia imetumia fedha nyingi sana kwa ajili ya kueneza fikra zake za kiwahabi na kitakfiri. Miongoni mwa sababu za hatua hiyo ya watawala wa Aal Saudi ni kwamba, Tunisia ilikuwa nchi ya kwanza ya Kiarabu ambayo mtawala wake dikteta aliondolewa madarakani hapo mwaka 2011. Kwa msingi huo Saudi Arabia imefanya jitihada kubwa za kuwekeza sana katika shule na taasisi za elimu nchini humo na kueneza fikra na mitazamo ya kiwahabi na kisalafi kwa shabaha ya kuitangaza nchi hiyo kuwa mfano wa kuigwa kwa nchi nyingine za Kirabu. Hata hivyo na licha ya uhusiano tuseme wa karibu baina ya Tunisia na serikali na Saudi Arabia, si tu kwamba fikra za kiwahabi zimekataliwa na wasomi bali hata baadhi ya viongozi wa serikali ya Tunis na wanafikra wa nchi hiyo wamekosoa waziwazi jitihada zinazofanywa na Saudia kueneza uwahabi nchini humo na kusema kuwa ugaidi ndiyo matunda na matokeo ya fikra za kiwahabi.

Image Caption

Katika mkondo huo tarehe 3 Novemba Waziri wa zamani wa Masuala ya Kidini wa Tunisia, Abdul Jalil bin Salim alisema katika kikao cha Bunge la nchi hiyo kilichohudhuriwa pia na balozi wa Saudi Arabia na mafisa wengine wa nchi hiyo kwamba shule za kidini za kisalafi nchini Saudia ndizo zinazotoa mafundisho na miongozi ya itikadi zenye misimamo ya kufurutu mipaka katika eneo la Mashariki ya Kati na kaskazini mwa Afrika. Katika kikao hicho Bin Salim alimtaka balozi wa Saudi Arabia nchini Tunisia na Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Mambo ya Ndani wa nchi za Kiarabu ambaye pia ni Msaudia, kuzifanyia marekebisho shule za kidini za Saudia kwa sababu ugaidi unatokana na mafunzo yanayotolewa katika shule hizo.

Magaidi wa kundi la Daesh wakijitayarisha kukatwa vichwa vya watu

Japokuwa serikali ya Tunisia ilimfuta kazi waziri Abdul Jalil bin Salim baada ya kukosoa fikra za kiwahabi za Saudia, lakini hapana shaka kuwa, matamshi hayo ni miongoni mwa ishara za ugumba na kutokuwa na matunda fikra za kisalafi nchini Tunsia.

Siku chache zilizopita pia Abdul Fattah Moro ambaye ni miongoni mwa waasisi wa harakati ya al Nahdha na Naibu Spika wa Bunge la Tunsia alisema kuwa uwahabi ndio msingi wa fikra za kundi la kigaidi la Daesh na kwamba Saudi Arabia ndio chanzo na mwanzilishi wa kundi hilo. Wakati huo huo mwandishi maarufu wa Tunisia, Badri al Madani, Oktoba mwaka huu aliitaja serikali ya Saudia kuwa ni ya kijahilia na kuongeza kuwa: Utawala wa kifalme wa Aal Saudi unahatarisha Uislamu, na kwamba vyombo vya habari vya kijahilia vya Waarabu vinazuia jamii ya Waislamu isipate na kujua ukweli na uhakika wa mambo.

Mkutano wa Umoja wa Kiislamu Tehran umelaani fikra za kitakfiri

Sheikh Muhammad Kaiwah ambaye ni miongoni mwa wanazuoni wa al Azhar na mhadhiri wa sayansi ya siasa katika Chuo Kikuu cha al Zaituna nhini Tunsia, Novemba mwaka huu alisema kuwa, Uislamu uko mbali kabisa na fikra za kitakfiri na kiwahabi. Msomi huyo amesisitiza kuwa: Idadi ya watu wanaohuburi na kueneza uwahabi nchini Tunisia imepungua na waliobakia sasa wanafanya kazi zao kwa siri.         

Tags