Askari 260 za Jenerali Haftar wameuawa Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22636-askari_260_za_jenerali_haftar_wameuawa_libya
Jeshi la wapiganaji wanaopinga Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya limetangaza kuwa, zaidi ya askari wake 260 wameuawa katika mapigano ya mji wa Benghazi huko mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 02, 2017 02:21 UTC
  • Askari 260 za Jenerali Haftar wameuawa Libya

Jeshi la wapiganaji wanaopinga Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya limetangaza kuwa, zaidi ya askari wake 260 wameuawa katika mapigano ya mji wa Benghazi huko mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na jeshi linaloongozwa na Jenerali Khalifa Haftar imesema kuwa, askari wake 268 wameuawa na wengine zaidi ya 500 kujeruhiwa katika mapigano ya mwaka uliopita wa 2016 katika mji wa Benghazi.

Jeshi hilo la Khalifa Haftar lilianza operesheni zake katika mji wa Benghazi mwaka 2014. Jeshi hilo liko chini ya Bunge la Tobruk ambao linapingana na Bunge la Serikali ya Umoja wa kitaifa mjini Tripoli.

Haftar

Jenerali Khalifa haftar

Katika miezi ya hivi karibuni jeshi hilo la Jenerali Khalifa Haftar limepata mafanikio makubwa katika mji wa Benghazi uliokuwa ukidhibitiwa na makundi ya kigaidi na vilevile katika maeneo yenye utajiri wa mafuta ya Libya.

Libya ilitumbukia katika machafuko ya ndani tangu baada ya kuondolewa madarakani utawala wa kidikteta wa Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.