Kujiuzulu Makamu wa Rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i22699-kujiuzulu_makamu_wa_rais_wa_serikali_ya_umoja_wa_kitaifa_ya_libya
Makamu wa Rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amejizulu wadhifa wake.
(last modified 2026-02-25T03:34:48+00:00 )
Jan 03, 2017 02:56 UTC
  • Kujiuzulu Makamu wa Rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya

Makamu wa Rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amejizulu wadhifa wake.

Habari zinasema kuwa baada ya kujiuzulu wadhifa huo, Musa al Koni  Makamu wa Rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya amewaomba radhi wananchi kwa kile alichokitaja kuwa kufeli katika utendaji wake wa kazi. Al Koni ameongeza kuwa amejiuzulu wadhifa huo kufuatia utawala wa Tripoli kushindwa kutatua matatizo ya wananchi tangu uingie madarakani mwezi Machi mwaka jana. 

Musa al Koni makamu wa Rais wa Libya aliyejiuzulu kutokana na kushindwa serikali kuwatumikia wananchi 

Ameongeza kuwa kujiuzulu kwake kumesababishwa na kushindwa baraza la uongozi katika kutatua matatizo na masaibu ya wananchi. Hii ni kwa sababu baraza hilo linabeba dhima ya kuuliwa, kutekwa nyara na kubakwa raia; vitendo vilivyotekelezwa huko Libya katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.