Waislamu wa Nigeria wamtaka Rais wa nchi hiyo amwachie huru Zakzaky
Mwanachama wa ngazi ya juu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amemtahadharisha Rais wa nchi hiyo baada ya kuakhirishwa zoezi la kumuachia huru kiongozi wa harakati hiyo anayeendelea kushikiliwa na vyombo vya usalama.
Nuruddin Musa, mwanachama wa ngazi ya juu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria leo amemtahadharisha Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo na kusema kuwa kuachiwa huru haraka iwezekanavyo kiongozi wao Sheikh Ibrahim Zakzaky pamoja na mkewe ni mstari mwekundu wa harakati hiyo na kwamba Harakati ya Kiislamu ya Nigeria haitakaa kimya kuhusu suala hilo.
Waislamu wengi wa Kishia wa Nigeria pia wamesisitiza udharura wa kutekelezwa haraka iwezekanavyo hukumu iliyotolewa na mahakama nchi hiyo ikitaka kuachiwa huru Sheikh Zakzaky na mkewe hadi mwisho wa muda wa kazi hii leo. Hukumu hiyo rasmi iliyotolewa na mahakama ya Nigeria inawaagiza polisi nchini humo kuandaa utangulizi wa kumuachia huru Sheikh Zakzaky na mke wake.
Jeshi la Nigeria tarehe 14 mwezi Disemba mwaka juzi lilimtia mbaroni Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe baada ya kuwauwa shahidi mamia ya wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo waliokuwa kwenye shughuli ya kidini katika mji wa Zaria.