Magaidi wa Boko Haram washambulia Niger na kuua askari wawili
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i24076-magaidi_wa_boko_haram_washambulia_niger_na_kuua_askari_wawili
Magaidi wa Boko Haram wametekeleza shambulizi la kushtukiza katika kituo kimoja cha kijeshi nchini Niger na kuua wanajeshi wawili. Kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Niger, shambulizi hilo limejiri katika kituo cha kijeshi kilichoko mjini Geskerou katika eneo la Diffa kusini mashariki mwa nchi hiyo. Katika shambulizi hilo magaidi hao wa Boko Haram ambao waliingia Niger wakitokea Nigeria, waliteketeza pia magari matatu ya jeshi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 22, 2017 12:44 UTC
  • Magaidi wa Boko Haram washambulia Niger na kuua askari wawili

Magaidi wa Boko Haram wametekeleza shambulizi la kushtukiza katika kituo kimoja cha kijeshi nchini Niger na kuua wanajeshi wawili. Kwa mujibu wa maafisa wa serikali ya Niger, shambulizi hilo limejiri katika kituo cha kijeshi kilichoko mjini Geskerou katika eneo la Diffa kusini mashariki mwa nchi hiyo. Katika shambulizi hilo magaidi hao wa Boko Haram ambao waliingia Niger wakitokea Nigeria, waliteketeza pia magari matatu ya jeshi.

Katika kujibu mapigo, jeshi la Niger lilitekeleza mashambulizi ya anga katika eneo la Ziwa Chad ambapo imearifiwa kuwa idadi kubwa ya magaidi wa Boko Haram wameuawa walipokuwa wakitoroka. Ziwa Chad liko katika nchi za Niger, Chad na Nigeria.

Wanamgambo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Boko Haram

Neno Boko Haram kwa ya lugha ya Kihausa inayotumiwa na Waislamu wengi Nigeria lina maana ya 'elimu kutoka nchi za Magharibi ni haramu'. Kundi hilo la Boko Haram ambalo lina ufahamu usio sahihi na potovu kuhusu dini ya Kiislamu, limekuwa likitekeleza hujuma katika maeneo mbalimbali ya Nigeria hasa kaskazini mwa nchi hiyo. Tokea kundi hilo lianzishe uasi mwaka 2009 hadi sasa, takribani watu 20,000 wameuawa na wengine takribani milioni mbili wamelazimika kuhama makazi yao.