Libya yaiomba Nato msaada wa kijeshi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25224-libya_yaiomba_nato_msaada_wa_kijeshi
Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imeuomba Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) usaidie kuimarisha majeshi yake.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Feb 16, 2017 15:44 UTC
  • Libya yaiomba Nato msaada wa kijeshi

Serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa imeuomba Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) usaidie kuimarisha majeshi yake.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Jens Stoltenberg, Katibu Mkuu wa Nato amesema kuwa muungano huo ulipokea ombi la Libya jana na kwamba sasa wanalichunguza ombi hilo na kuona ni msaada gani wanaoweza kuipatia serikali ya Libya.

Katibu Mkuu wa Muungano wa NATO, Jens Stoltenberg

Miongoni mwa misaada iliyoombwa na serikali ya Libya ni kuanzisha taasisi na idara za usalama na ulinzi nchini humo.

Libya ilitumbukia katika hali ya mchafukoge baada ya kuondolewa madarakani dikteta wa zamani wa nchi hiyo Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011. Harakati na makundi mbalimbali yanayobeba silaha pia yameshadidisha mapigano huko Libya.

Hivi sasa Libya ina serikali mbili; moja ikiwa na makao makuu katika mji wa Tobruk mashariki mwa nchi hiyo, na nyingine ikiendeshwa na Kongresi ya Taifa ya nchi hiyo mjini Tripoli.