Juhudi za Rais wa Sudan Kusini za kurejesha amani nchini
(last modified Wed, 22 Feb 2017 07:54:48 GMT )
Feb 22, 2017 07:54 UTC
  • Juhudi za Rais wa Sudan Kusini za kurejesha amani nchini

Rais wa Sudan Kusini ameyatolea mwito makundi ya kisiasa nchini humo kujiunga na mazungumzo ya kitaifa.

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini jana aliyataka makundi ya kisiasa ya upinzani kujiunga katika mazungumzo ya kitaifa ili kurejesha amani nchini humo. Rais Kiir amesema kuwa mazungumzo ya pamoja ya kisiasa yanaweza kusaidia kurejeshwa amani huko Sudan Kusini na kuongeza kuwa mazungumzo ya kitaifa ni kipaumbele cha serikali yake. Rais wa Sudan Kusini ameashiria pia kuwa mazungumzo ya kitaifa yanaweza kuzidisha kiwango cha umoja kati ya wananchi na kwamba kuwepo umoja wa kitaifa pia utapelekea kuongezeka hali ya usalama nchini humo. 

Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini mwezi Disemba mwaka jana alitangaza kufanyika mazungumzo ya kitaifa kwa lengo la kuhitimisha vita vya ndani vya miongo mitatu nchini humo. Sudan Kusini inakabiliwa na mapiganoo kati ya wafuasi wa Rais Kiir na wale wa Makamu wake wa zamani Riek Machar tangu mwezi Disemba mwaka 2013 hadi sasa.

Riek Machar, Makamu wa zamani wa Rais wa Sudan Kusini ambaye ni kiongozi wa waasi wa nchi hiyo 

Pande hizo zinazozozana zilisaini makubaliano ya kusimamisha mapigano mwezi Agosti mwaka juzi, hata hivyo kuanzia msimu wa joto mwaka jana hadi hivi sasa, mapigano yameanza tena kati ya pande hizo hasimu. Vita hivyo vya ndani vimesababisha raia milioni tatu kuwa wakimbizi katika nchi jirani.