Misri yataka mikono ya kigeni isiingilie masuala ya ndani ya Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25570-misri_yataka_mikono_ya_kigeni_isiingilie_masuala_ya_ndani_ya_libya
Serikali ya Misri imesema, kuna wajibu wa kufanyika juhudi za kutosha za kuwasaidia Walibya kutatua migogoro yao, lakini bila ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 24, 2017 04:41 UTC
  •  Fayez al Sarraj, rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya
    Fayez al Sarraj, rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya

Serikali ya Misri imesema, kuna wajibu wa kufanyika juhudi za kutosha za kuwasaidia Walibya kutatua migogoro yao, lakini bila ya kuingilia masuala ya ndani ya nchi hiyo.

Katika mazungumzo yake ya simu na Fayez al Sarraj, rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya, Sameh Shokri, Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema, utatuzi wa kisiasa wa mgogoro wa Libya utapatikana kwa maamuzi ya wananchi wenyewe wa Libya chini ya fremu ya kulinda uhuru na haki ya kujitawala nchi hiyo bila ya uingiliaji wa nchi ajinabi.

Katika  mazungumzo hayo ya simu Shokri amemuhakikisha rais wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya kuwa Misri itaendelea na juhudi zake za kuyapatanisha makundi mbalimbali ya Libya hadi utakapopatikana ufumbuzi wa kweli wa kisiasa wa mgogoro wa nchi hiyo.

 

Aidha Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri imesema, pande hizo mbili zimezungumzia pia matokeo ya kikao cha pande kadhaa cha kuutatufita ufumbuzi mgogoro wa Misri kilichofanyika tarehe 20 mwezi huu wa Februari na kuzishirikisha nchi za Tunisia, Misri na Algeria mjini Tunis.

Libya imetumbukia kwenye mgogoro mkubwa tangu mwaka 2011 kutokana na uingiliaji wa kigeni hususan Shirika la Kijeshi la Nchi za Magharibi NATO, katika kampeni za kuungóa madarakani utawala wa Kanali Muammar Gaddafi, na hadi hivi sasa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika imeshindwa kuwa na utulivu.