Mawakili wa Zakzaky wamwandikia barua Mwanasheria Mkuu, Waziri
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i25740-mawakili_wa_zakzaky_wamwandikia_barua_mwanasheria_mkuu_waziri
Mawakili wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wamemuandikia barua Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Sheria wa nchi hiyo, wakishinikiza kuachiwa huru msomi huyo wa Kiislamu pamoja na mkewe.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 28, 2017 04:19 UTC
  • Mawakili wa Zakzaky wamwandikia barua Mwanasheria Mkuu, Waziri

Mawakili wa Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria wamemuandikia barua Mwanasheria Mkuu na Waziri wa Sheria wa nchi hiyo, wakishinikiza kuachiwa huru msomi huyo wa Kiislamu pamoja na mkewe.

Mawakili hao wanasema licha ya kupita miezi miwili tangu Mahakama Kuu ya Federali ya nchi hiyo kuagiza kuachiwa huru Sheikh Zakzaky na mkewe kufikia Januari 16 mwaka huu, lakini vyombo vya usalama vimekataa kuwaachia huru na kuendelea kuwazuilia kinyume cha katiba.

Mawakili hao wamesema katika barua yao hiyo kuwa, kuendelea kuzuiliwa Sheikh Zakzaky na mkewe licha ya kupita muda wa makatakaa iliyotolewa na mahakama Disemba 2, ni ukiukaji mkubwa wa mfumo wa sheria.

Waislamu Nigeria wamekuwa wakiandamana mara kwa mara kushinikiza kuachiwa huru Sheikh Zakzaky

Hii ni katika hali ambayo, duru za habari zimeiarifu taasisi ya IHRC kuwa, tayari Mwanasheria Mkuu wa Nigeria, Malami Abubakar, ameidhinisha ombi la kuhamishiwa Sheikh Zakzaky jimbo la Kaduna, kwa ajili ya kusikiliza kesi dhidi yake, kwa tuhuma zinazorejea nyuma hadi miongo mitatu iliyopita.

Waislamu wa Nigeria wamewasilisha kilio chao cha kutaka kuachiwa huru Sheikh Zakzaky na mkewe, kwa Makamu wa Rais wa nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika, Yemi Osimbaji.