Ladsous: Hali ya usalama nchini Mali inatia wasiwasi
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anayehusika na Oparesheni za Kudumisha Amani za huo amesema kuwa hali ya usalama nchini humo inatia wasiwasi.
Herve Ladsous ameeleza kuwa hali ya usalama nchini humo ingali inatia wasiwasi licha ya kutumwa wanajeshi hao wa Umoja wa Mataifa na kupatikana mafanikio ya kiwango fulani katika kufikiwa makubaliano ya kusaka amani nchini humo. Ladsous ameeleza kuwa mashambulizi na harakati za makundi yenye silaha huko Mali hayajapungua.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Anayehusika na Oparesheni za Kudumisha amani ameongeza kuwa makubaliano ya amani yaliyosainiwa mwezi Juni mwaka 2015 kati ya serikali ya Mali, waungaji mkono wa serikali hiyo na waasi wanaoendesha harakati zao kaskazini mwa nchi hiyo pia yameshindwa kurejesha amani nchini humo. Kikosi cha kudumisha amani cha UN ambacho kilielekea Mali tangu Julai mwaka 2013, hadi sasa kimepoteza wanajeshi wake zaidi ya 70. Idadi hiyo ya wanajeshi waliouawa inatajwa kuwa kubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa kwa wanajeshi wa kulinda amani.