Kiongozi wa Daesh auawa mashariki mwa Algeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i26884-kiongozi_wa_daesh_auawa_mashariki_mwa_algeria
Jeshi la Algeria limetangaza habari ya kuuawa kiongozi mmoja wa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) katika eneo la Jabal al Wuhush la jimbo la Constantine, mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 26, 2017 13:23 UTC
  • Kiongozi wa Daesh auawa mashariki mwa Algeria

Jeshi la Algeria limetangaza habari ya kuuawa kiongozi mmoja wa genge la kigaidi la Daesh (ISIS) katika eneo la Jabal al Wuhush la jimbo la Constantine, mashariki mwa nchi hiyo.

Jeshi la Algeria limetangaza habari hiyo leo na kuongeza kuwa, katika operesheni yake maalumu, jeshi hilo limefanikiwa kumuua kiongozi wa kundi la Daesh anayejulikana kwa jina la Abul Hammam, kamanda wa brigedi ya al Ghurabaa ambayo mwaka jana ilitangaza rasmi kuwa ni tawi la genge la kigaidi la ISIS.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, jeshi la Algeria limefanikiwa pia kukamata silaha aliyokuwa nayo afisa mmoja wa polisi aliyeuliwa na Daeshi mwezi Oktoba mwaka jana katika vifaa alivyokutwa navyo kamanda huyo wa brigedi ya al Ghurabaa anayejulikana kwa jina la kupanga la Abul Hammam.

Genge la kigaidi la Daesh

 

Kabla ya hapo magaidi wa Daeshi walitangaza kuhusika katika opereseheni iliyofeli ya kushambulia kituo cha polisi la mji wa Constantine mwezi uliopita wa Februari. Maafisa wawili wa polisi waliuawa kwenye shambulio hilo la kigaidi ambapo gaidi aliyefanya shambulio hilo naye aliuawa papo hapo.

Mwaka 2016 vikosi vya ulinzi vya Algeria vilifanikiwa kuangamiza magaidi 125 na kuwatia mbaroni wengine 225 na kugundua ghala moja kubwa la silaha za magaidi hao.

Tangu mwanzoni mwa mwaka huu hadi hivi sasa, jeshi la Algeria limeshaua magaidi 37 katika nyakati tofauti.