Wahajiri karibu 100 watoweka pwani ya Libya
Apr 14, 2017 03:03 UTC
Karibu wahamiaji 100 wametoweka baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kuzama katika maji ya pwani mwa Libya wakiwa mbioni kuelekea Ulaya.
Boti hiyo imezama katika maji ya pwani mwa eneo la Gargaresh. Msemaji wa Gadi ya Pwani mwa Libya, Ayoub Qassem amesema kuwa boti hiyo ilipasuka na kuzama na kwamba wahajiri 27 kati ya waliokuwemo ndani ya boti hiyo wameokolewa na wengine 97 hawajulikani waliko.
Libya imeendelea kuwa lango linalotumiwa na wahajiri haramu kuelekea barani Ulaya kupitia njia hatari ya Bahari ya Mediterania. Tangu mwanzoni mwa mwaka huu pekee wahajiri zaidi ya 600 wamezama na kufa maji katika bahari ya Mediterania.
Tags