Katibu Mkuu wa UN atahadharisha kuwa Daesh wanaweza kuidhibiti tena Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i27788-katibu_mkuu_wa_un_atahadharisha_kuwa_daesh_wanaweza_kuidhibiti_tena_libya
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu hatari ya kupanuka zaidi udhibiti wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika maeneo mbalimbali ya Libya na hali mbaya inayotawala maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Apr 15, 2017 00:17 UTC
  • Katibu Mkuu wa UN atahadharisha kuwa Daesh wanaweza kuidhibiti tena Libya

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametahadharisha kuhusu hatari ya kupanuka zaidi udhibiti wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika maeneo mbalimbali ya Libya na hali mbaya inayotawala maeneo yanayodhibitiwa na kundi hilo.

António Guterres amesema kuwa, ana wasiwasi kuhusu harakati zinazoshadidi na ukatili mpya unaofanywa na wanachama wa kundi hilo nchini Libya na vilevile mkwamo wa kisiasa unaoshuhudiwa nchini humo.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, licha ya kuwa kundi la Daesh halidhibiti kikamlifu eneo lolote la Libya lakini wanachama wake wanaendeleza harakati zao katika ardhi ya nchi hiyo na wanaendelea kufanya mashambulizi katika maeneo mbalimbali. 

Wapiganaji wa Daesh wakiwa tayari kukata vichwa vya wahanga wao, Libya

Kundi la kigaidi na kiwahabi la Daesh Julai 2015 lilivamia na kuteka miji mingi ya Libya kutokana na ombwe wa kisiasa na kiutawala unaoendelea kuisumbua nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Wanachama wa kundi hilo wangali wanaendesha harakati zao katika maeneo mbalimbali ya Libya licha ya kufukuzwa katika mji wa Sirte Disemba mwaka jana.