Morocco yaituhumu Algeria kuwatesa wakimbizi wa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i28144-morocco_yaituhumu_algeria_kuwatesa_wakimbizi_wa_syria
Serikali ya Morocco imeilaumu Algeria kwa kuwazingira wakimbizi wa Syria katika "mazingira yasiyo ya kibinadamu" kwenye mpaka wa kusini mwa Algeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 23, 2017 03:24 UTC
  • Morocco yaituhumu Algeria kuwatesa wakimbizi wa Syria

Serikali ya Morocco imeilaumu Algeria kwa kuwazingira wakimbizi wa Syria katika "mazingira yasiyo ya kibinadamu" kwenye mpaka wa kusini mwa Algeria.

Mtandao wa habari wa gazeti la al Quds al Arabi umeripoti habari hiyo kwa kuinukuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco ikilaani kile ilichokiita ni vitendo visivyo vya kibinadamu vinavyofanywa na Algeria dhidi ya wakimbizi wa Syria kwenye mpaka wa kusini wa nchi hiyo.

Wakimbizi wa Syria

 

Taarifa ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Morocco imesema, maafisa wa Algeria wamewazuia na kuwazingira kila upande wakimbizi 55 wa Syria katika mpaka wa kusini mashariki mwa nchi hiyo licha ya kwamba waliridhia wakimbizi hao kuingia katika mji wa Figuig (Fajij).

Hadi tunapokea habari hii, Algeria ilikuwa haijasema lolote kuhusiana na tuhuma hizo za viongozi wa Morocco.

Ikumbukwe kuwa mpaka wa Algeria na Morocco umefungwa tangu mwaka 1994 kutokana na sababu tofauti.