Libya yataka mashambulizi ya jeshi la Misri nchini humo kufuatiliwa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i29784-libya_yataka_mashambulizi_ya_jeshi_la_misri_nchini_humo_kufuatiliwa_kimataifa
Wabunge la Libya wametaka kufuatiliwa katika asasi za kimataifa mashambulizi ya anga ya Misri ndani ya ardhi ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 30, 2017 03:25 UTC
  • Libya yataka mashambulizi ya jeshi la Misri nchini humo kufuatiliwa kimataifa

Wabunge la Libya wametaka kufuatiliwa katika asasi za kimataifa mashambulizi ya anga ya Misri ndani ya ardhi ya nchi hiyo.

Taarifa iliyotolewa na wawakilishi hao, imelitaka baraza la uongozi nchini humo kuwasilisha rasmi mashtaka ya Libya katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na asasi nyingine za kimataifa juu ya mashambulizi hayo ya Misri. Aidha wamebainisha kuwa, shambulizi hilo la anga la Misri nchini Libya lililofanywa kwa kisingizio cha kupamabana na ugaidi bila kutoa dalili za kutosha kwa viongozi wa taifa hilo haliwezi kukubalika.

Ndege za Misri zikiwa katika anga ya Libya kuwashambulia magaidi

Kuhusiana na suala hilo, wabunge hao wametoa onyo kwa Cairo juu ya kukariri kwake hatua hizo kama ambavyo pia wameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Libya chini ya serikali ya umoja wa kitaifa kumwita balozi wa Misri nchini humo na kumlalamikia kuhusu suala hilo. Hayo yanajiri katika hali ambayo mapema jana kundi la Ikhwanul Muslimin lililopigwa marufuku nchini Misri, lilitoa taarifa ya kulaani mashambulizi ya nchi hiyo huko Libya. Taarifa iliyotolewa na kundi hilo ilisema kuwa, shambulizi hilo la ndege za jeshi la Misri, limetokana na kushindwa serikali ya Cairo katika kuwashika wahusika wa shambulizi la mji wa Minya.

Wanachama wa kundi la kigaidi la Daesh (ISIS) nchini Libya

Kadhalika ripoti hiyo ya Ikhwanul Muslimin imeongeza kuwa, hatua hiyo ya Misri dhidi ya Libya itaongeza uhasama na nchi hiyo jirani.