Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran barani Afrika
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i30612
Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo (Jumapili) anaanza ziara ya kuzitembelea nchi za Algeria, Mauritania na Tunisia.
(last modified 2025-07-19T08:58:23+00:00 )
Jun 18, 2017 03:52 UTC
  • Safari ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran barani Afrika

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo (Jumapili) anaanza ziara ya kuzitembelea nchi za Algeria, Mauritania na Tunisia.

Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, Mohammad Javad Zarif ameamua kuzitembelea nchi za Algeria, Mauritania na Tunisia baada ya kupokea mwaliko kutoka kwa viongozi wa nchi hizo. Akiwa katika nchi hizo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ataonana na mawaziri wenzake wa mambo ya nje pamoja na marais wa nchi hizo tatu za kaskazini mwa Afrika.

 

Qassemi amesema, lengo na shabaha ya safari hiyo ya siku mbili ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran ni kuimarisha uhusiano wa pande mbili na pande kadhaa. Ameongeza kuwa, katika safari hiyo, Mohammad Javad Zarif atazungumza pia na viongozi wa nchi hizo tatu masuala ya kieneo ikiwemo kadhia ya Syria na masuala mengine ya Ghuba ya Uajemi.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran pia amesema, matukio yanayojiri hivi sasa yanahitajia kufanyike mazungumzo zaidi baina ya nchi za eneo hili na kwamba Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inaamini kuwa nchi za Kiislamu zinapaswa kushikamana, kuungana na kuwa kitu kimoja hivi sasa kuliko wakati mwingine wowote. Pia ziongoze ushirikiano baina yao kwa ajili ya kupambana na njama za maadui wanaofanya njama za kila namna za kuzusha mizozo na mifarakano katika safu za Waislamu.