Jun 22, 2017 08:03 UTC
  • Shirika la Msalaba Mwekundu latahadharisha kuhusu hali ya Nigeria

Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limetangaza kuwa, hali ya kibinadamu nchini Nigeria inatia wasiwasi licha ya juhudi kubwa zilizofanywa na serikali ya nchi hiyo.

Mratibu wa mawasiliano wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu nchini Nigeria, Aleksandra Matijevic amesema juhudi zilizofanywa na serikali ya Nigeria kwa ajili ya kukabiliana na mgogoro wa kibinadamu nchini humo katika mwaka uliopita wa 2016 hazitoshi na kwamba, mapigano ya ndani huko mashariki mwa Nigeria ambayo sasa yamehamia katika nchi jirani, yangali yanaendelea.

Afisa huyo wa Shirika la Msalaba Mwekundu ameeleza wasiwasi wake kuhusu hali ya wakimbizi wanaoishi katika maeneo ambako misaada ya kibinadamu haifiki kutokana na ukosefu wa amani.

Baadhi ya wakimbizi kaskazini mashariki maa Nigeria

Takwimu za Umoja wa Mataifa zinasema kuwa, Wanigeria milioni 14 wanahitajia misaada ya kibinadamu. Harakati za kundi la kigaidi la Boko Haram zimeathiri maisha ya Wanigeria milioni 26 katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Watu elfu 20 wameuawa na mamilioni ya wengine wamelazimika kuwa wakimbizi kutokana na amshambulizi yanayoendelea kufanywa na wanachama wa kundi la kigaidi na kiwahabi la Boko Haram katika maeneo hayo.    

Tags