Algeria: Waafrika elfu tano wamejiunga na makundi ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i31328-algeria_waafrika_elfu_tano_wamejiunga_na_makundi_ya_kigaidi
Rais wa Algeria ametahadharisha kuhusu hatari ya vijana elfu tano wa Afrika waliojiunga na mkundi ya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 04, 2017 08:13 UTC
  • Algeria: Waafrika elfu tano wamejiunga na makundi ya kigaidi

Rais wa Algeria ametahadharisha kuhusu hatari ya vijana elfu tano wa Afrika waliojiunga na mkundi ya kigaidi.

Rais Abdelaziz Bouteflika wa Algeria ameyasema hayo katika ujumbe wake uliosomwa kwenye mkutano wa viongozi wa Afrika unaofanyika mjini Addis Ababa, Ethiopia na kuongeza kuwa: Vijana wengi wa nchi za Afrika wamejiunga na makundi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali duniani hususan Iraq, Syria na eneo la Sahel kaskazini mwa Afrika.

Amesema kuwa, nchi za Afrika zinakabiliwa na changamoto kubwa kutokana na uwezekano wa magaidi wa Kiafrika kurejea katika nchi zao na ametoa wito wa kuwepo ushirikiano katika masuala ya kiusalama na upelelezi kwa ajili ya kudhibiti vyema mipaka na kuzuia harakati za magaidi. 

Mkutano wa AU, Addis Ababa

Kwa miaka kadhaa sasa makundi ya kigaidi kama Daesh yaliyoanzishwa kwa ufadhili na misaada ya hali na mali ya Marekani, Saudi Arabia, Israel na washirika wao yamekuwa yakifanya mashambulizi katika nchi mbalimbali duniani hususan katika nchi za Syria na Iraq. Makundi hayo yamesajili wapiganaji kutoka nchi nyingi zikiwemo za Afrika.

Mkutano wa 29 wa viongozi wa nchi za Afrika ulianza jana katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa. Zaidi ya viongozi 25 wa nchi za Afrika wanahudhuria mkutano huo.