Mbabe wa kivita wa Kongo ajisalimisha kwa wanajeshi wa UN
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i32328-mbabe_wa_kivita_wa_kongo_ajisalimisha_kwa_wanajeshi_wa_un
Ntabo Ntaberi Sheka mmoja wa wababe hatari wa kivita waliokuwa wakisakwa kwa udi na uvumba wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa jinai dhidi ya binadamu amejisalimisha kwa Umoja wa Mataifa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 27, 2017 03:15 UTC
  • Mbabe wa kivita wa Kongo ajisalimisha kwa wanajeshi wa UN

Ntabo Ntaberi Sheka mmoja wa wababe hatari wa kivita waliokuwa wakisakwa kwa udi na uvumba wa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa jinai dhidi ya binadamu amejisalimisha kwa Umoja wa Mataifa.

Wanamgambo wanaoongozwa na mbabe huyo wa kivita kwa jina la Mai-Mai Sheka ni tawi la makundi yanayobeba silaha huko mashariki mwa Kongo ambayo mara mara yamekuwa yakituhumiwa na Umoja wa Mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwa kutumia vitendo vya ubakaji kama silaha yao ya kivita.

Mbabe wa kivita Ntabo Ntaberi Sheke akiwa huko Walikale mwaka 2011  

Baada ya kujificha na kusakwa kwa muda wa miaka sita, Sheka hatimaye amejisalimisha kwa vikosi vya Umoja wa Mataifa katika mji wa Mutongo katika eneo la Walikale na kusafirishwa hadi katika mji wa Goma mashariki mwa nchi. Hayo yameelezwa na Fabienne Pompey msemaji wa kikosi cha MONUSCO. Mbabe huyo wa kivita aliyejisalimisha anatazamiwa kukabidhiwa kwa maafisa wa Kongo baada ya taratibu kukamilika.