Upinzani Kenya kuieleza mahakama jinsi teknolojia ilivyowezesha wizi wa kura
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i33494-upinzani_kenya_kuieleza_mahakama_jinsi_teknolojia_ilivyowezesha_wizi_wa_kura
Mrengo wa upinzani nchini Kenya umesema kuwa utathibitisha mbele ya Mahakama ya Kilele ya nchi hiyo kwamba teknolojia ilifanikisha kuliko kuzuia wizi wa kura wakati wa uchaguzi mkuu nchini humo hivi karibuni, ikiwa ni katika juhudi za mrengo huo za kutaka kubadilisha kura alizoshinda Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi huo uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.
(last modified 2026-03-03T16:16:59+00:00 )
Aug 22, 2017 15:30 UTC
  • Upinzani Kenya kuieleza mahakama jinsi teknolojia ilivyowezesha wizi wa kura

Mrengo wa upinzani nchini Kenya umesema kuwa utathibitisha mbele ya Mahakama ya Kilele ya nchi hiyo kwamba teknolojia ilifanikisha kuliko kuzuia wizi wa kura wakati wa uchaguzi mkuu nchini humo hivi karibuni, ikiwa ni katika juhudi za mrengo huo za kutaka kubadilisha kura alizoshinda Rais Uhuru Kenyatta katika uchaguzi huo uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu.

Kiongozi wa Muungano wa upinzani Kenya NASA, Raila Odinga  amesema katika malalamiko waliyowasilisha Ijumaa iliyopita kwamba, matokeo ya uchaguzi yaliyokusanywa kutoka vituo vya kupigia kura zaidi ya theluthi moja yalichachakuliwa kwa kiasi kikubwa kutokana na kuwepo kwa kasoro katika mfumo kielektroniki unaosambaza makaratasi ya matokeo ya kura.

Raila Odinga Kiongozi wa Muungano wa Upinzani wa (NASA)

Maafisa wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC)  wametangaza kuwa Uhuru Kenyatta aliyekuwa mgombea wa chama cha Jubilee katika uchaguzi wa Rais nchini Kenya uliofanyika tarehe Nane mwezi huu alimzidi mpinzani wake kwa kura milioni 1.4. Aidha matokeo mengine ya uchaguzi huo yaliyochapishwa na waangalizi wa kujitegemea baada ya kuhesabiwa kura katika vituo elfu mbili yalitoa takwimu sawa na hizo za IEBC. Wakati huo huo Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kenya ilitangaza kuwa watu wasiopungua 28 waliuawa katika machafuko yaliyosababishwa na ghasia za uchaguzi baada ya kumalizika uchaguzi khususan katika maeneo ambayo Odinga ana uungaji mkono mkubwa wa wananchi.

Moja ya nyaraka zilizowasilishwa na Muungano wa NASA inasomeka hivi: Mianya mingi iliyosababishwa kwa makusudi au kutokana na uzembe imetatiza kutumia vyema teknolojia ili kuwalisha mchakato sahihi wa utoaji matokeo. Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya imetakiwa kutoa jibu kwa mashtaka hadi kufikia Ijumaa wiki hii na kwamba kesi hiyo inatazamiwa kuanza Jumamosi ijayo. Naye George Kegoro Mkuu wa Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Kenya amesema uchaguzi wa mwaka huu nchini Kenya umefeli sawa kabisa na ule uliopita.