Upinzani Zimbabwe wakataa mpango wa kuasisi muungano wa kitaifa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i34013-upinzani_zimbabwe_wakataa_mpango_wa_kuasisi_muungano_wa_kitaifa
Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC) jana Jumatano kilieleza kuwa hakina mipango ya kujiunga na vijikundi vilivyopo ndani ya chama tawala ZANU-PF ili kuasisi muungano wa umoja wa kitaifa baada ya kuaga dunia Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo aliye na umri wa miaka 93.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Sep 06, 2017 23:51 UTC
  • Upinzani Zimbabwe wakataa mpango wa kuasisi muungano wa kitaifa

Chama cha upinzani nchini Zimbabwe cha Movement for Democratic Change (MDC) jana Jumatano kilieleza kuwa hakina mipango ya kujiunga na vijikundi vilivyopo ndani ya chama tawala ZANU-PF ili kuasisi muungano wa umoja wa kitaifa baada ya kuaga dunia Rais Robert Mugabe wa nchi hiyo aliye na umri wa miaka 93.

Uchunguzi wa Shirika la habari la Reuters wiki hii umebainisha kuwa Emmerson Mnangagwa Makamu wa Rais wa Zimbabwe ambaye anaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumrithi Mugabe amekuwa akifikiria kuanzisha muungano mkubwa ambao utasogeza mbele uchumi wa nchi hiyo kwa kuwaleta pamoja maelfu ya wakulima wazungu waliofukuzwa katika ardhi zao mapema mwaka 2000.  

Emmerson Mnangagwa, Makamu wa Rais wa Zimbabwe 

Ripoti hiyo imetegemea taarifa zilizovuja kutoka Taasisi Kuu ya Intelijinsia ya Zimbabwe pamoja na mahojiano waliyofanyiwa wanasiasa watajika akiwemo kiongozi wa chama cha MDC Morgan Tsvangirai. Chama cha MDC kimesema kuwa kamwe hakiwezi kufikiria kujiunga na utawala ambao haujatokana na uchaguzi. Uchaguzi mkuu ujao utafanyika mwakani na Robert Mugabe atapeperusha bendera ya chama cha ZANU-PF katika uchaguzi huo akiwania kiti cha urais.