Sisitizo la kuendelezwa mapambano ya Wapalestina dhidi ya maghasibu wa Kizayuni
Shakhsia na taasisi zisizo za kiserikali za nchini Algeria wamesisitiza kuendelezwa mapambano ya Wapalestina dhidi ya vitendo vya mabavu na ukandamizaji wa maghasibu wa Kizayuni.
Shakhsia wanamapinduzi wa Algeria na taasisi zisizo za kiserikali za nchini humo jana walitahadharisha kuhusu njama za utawala wa Kizayuni na baadhi ya serikali za Kiarabu kwa ajili ya kusahaulisha kufuatiliwa suala Palestina. Pande hizo zilitoa indhari hiyo katika hafla iliyofanyika chini ya anuani Siku ya Kimataifa ya Kuiunga Mkono Palestina".
Dakta Luay Issa Balozi wa Palestina nchini Algeria pia alisema katika marasimu hayo kuwa tatizo kuu la Wapalestina ni udhaifu wa nchi za Kiarabu katika kuyaunga mkono malengo na matarajio ya wananchi wa Palestina.
Balozi wa Palestina aliongeza kuwa juhudi zinafanywa ili kufuatilia kadhia ya Palestina katika taasisi za kimataifa. Katika hafla hiyo, Abdumajid Si-afif Mkuu wa Kamati ya Masuala ya Nje na Ushirikiano ya Bunge la Algeria ameeleza kuwa msimamo wa wananchi na serikali ya nchi hiyo kuhusu Palestina uko imara na si wa kujadiliwa.