Sudan Kusini kujiunga na Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Kemikali
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37087-sudan_kusini_kujiunga_na_mkataba_wa_kupiga_marufuku_silaha_za_kemikali
Sudan Kusini itakuwa nchi mwanachama wa Mkataba wa Silaha za Kemikali, CCW na kujiunga na Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali Duniani, OPCW.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 02, 2017 11:26 UTC
  • Sudan Kusini kujiunga na Mkataba wa Kupiga Marufuku Silaha za Kemikali

Sudan Kusini itakuwa nchi mwanachama wa Mkataba wa Silaha za Kemikali, CCW na kujiunga na Shirika la Kuzuia Silaha za Kemikali Duniani, OPCW.

Hayo yametangazwa na mkurugenzi mkuu wa ushirikiano wa kimataifa katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ya Sudan Kusini Moses Akol Ajawin kwenye kikao cha 22 cha Mkutano wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Silaha za Kemikali.

Naye mkurugenzi mkuu wa OPCW amepongeza uamuzi huo wa Sudan Kusini na kutaka nchi mbili ambazo ni Misri, na Korea Kaskazini pamoja na utawala haramu wa Israel ambazo hazijajiunga na Shirika hilo kuungana na wengine duniani katika kutokomeza silaha zote za kemikali.

Tokea mwaka 1997, nchi 192 zimetia saini mkataba wa kutokomeza silaha za kemikali na ziko katika mkakati wa kuangamiza silaha za kemikali chini ya usimamizi wa shirika la OPCW. Mwezi Aprili mwaka huu, Antonio Guterres Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa aliashiria namna hadi kufikia sasa karibu asilimia 95 ya akiba ya silaha za kemikali zilizotangazwa kuwepo duniani zimeshaharibiwa  na shirika hilo.