Wakimbizi 12,000 kutoka DRC waingia Zambia, UNHCR haina fedha za kuwashguhulikia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i37165-wakimbizi_12_000_kutoka_drc_waingia_zambia_unhcr_haina_fedha_za_kuwashguhulikia
Zaidi ya wakimbizi 12,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekimbilia nchi jirani ya Zambia kutafuta hifadhi kutokana na machafuko Kusini Mashariki mwa nchi yao.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Dec 04, 2017 07:39 UTC
  • Wakimbizi 12,000 kutoka DRC waingia Zambia, UNHCR haina fedha za kuwashguhulikia

Zaidi ya wakimbizi 12,000 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekimbilia nchi jirani ya Zambia kutafuta hifadhi kutokana na machafuko Kusini Mashariki mwa nchi yao.

Umoja wa Mataifa unaonya kuwa, hali ya wakimbizi hao ni mbaya na kwamba wanakosa mahitaji muhimu kwa sababu ya uhaba wa fedha na pia kuendelea kuongezeka kwa wakimbizi hao.

UNHCR inasema inahitaji dola za Marekani milioni 236 kuwasaidia wakimbizi hao.

Msemaji wa UNCHR Babar Baloch anasema katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita pekee, zaidi ya wakimbizi 8,400 wameingia nchini Zambia wengi wao wakiwa wanawake na watoto. Kuzorota usalama nchini DRC kumesababisha raia wengi kuyahama makazi yao.

Wakimbizi

Hayo yanajiri wakati ambapo chama kikuu cha upinzani nchini DRC, UDPS kinasema hakimtambui Waziri Mkuu Bruno Tshibala kama mwanachama na kiongozi ndani ya chama hicho.

Hatua hii inakuja baada ya Tshibala ambaye amewahi kuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho kusema kuwa anaandaa mkutano wa chama hicho kumteua kiongozi mpya wa UDPS baada ya kifo cha Ettien Tshisekedi mapema mwaka huu.