Maelfu ya wakimbizi wa Kongo wawasili Uganda
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i38195-maelfu_ya_wakimbizi_wa_kongo_wawasili_uganda
Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa kuanzia tarehe 18 mwezi huu hadi hivi sasa zaidi ya wakimbizi 4500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia Uganda.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 27, 2017 23:13 UTC
  • Maelfu ya wakimbizi wa Kongo wawasili Uganda

Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa limetangaza kuwa kuanzia tarehe 18 mwezi huu hadi hivi sasa zaidi ya wakimbizi 4500 kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo wamekimbilia Uganda.

Filippo Grandi Mkuu wa Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) ametangaza kuwa wengi wa wakimbizi hao wameingia Uganda kupitia ziwa Albat. Taarifa ya UNHCR imeongeza kuwa wakimbizi zaidi ya 1,860 wamesajiliwa kati ya tarehe 23 hadi 26 mwezi huu wa Disemba na hivyo kuifanya idadi ya wakimbizi waliowasili Uganda tangu tarehe 18 mwezi huu kufikia 4,584.  

Wakimbizi wa Kongo waliowasili Uganda wakikwepa machafuko nchini kwao 

Sehemu kubwa ya wakimbizi inaundwa na wanawake na watoto na hadi kufikia sasa mkimbizi mmoja ameripotiwa kuuawa miongoni mwa idadi hiyo. Maeneo ya katikati, mashariki na kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo yameathiriwa na machafuko kwa kwa miaka 20 sasan. Raia wa Kongo walioathiriwa na vita zaidi ya elfu tisa mwezi Aprili mwaka huu walikimbilia nchi jirani ya Angola kwa ajili ya hifadhi.