Walinda amani Sudan Kusini wakumbwa na kashfa ya kimaadili
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i40877-walinda_amani_sudan_kusini_wakumbwa_na_kashfa_ya_kimaadili
Baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanakabiliwa na tuhuma za kufanya ufisadi wa kimaadili katika mji wa Wau wa Sudan Kusini.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 26, 2018 03:51 UTC
  • Walinda amani Sudan Kusini wakumbwa na kashfa ya kimaadili

Baadhi ya walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanakabiliwa na tuhuma za kufanya ufisadi wa kimaadili katika mji wa Wau wa Sudan Kusini.

Shirika la habari la Associated Press limeinukuu ofisi ya walinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini ikisema kuwa, kundi moja la walinda amani 46 wameitwa mjini Juba baada ya kutuhumiwa kufanya ufisadi wa kimaadili katika mji wa Wau.

Umoja wa Matafia una askari 17 elfu wa kulinda amani huko Sudan Kusini.

Katika miaka ya hivi karibuni, Umoja wa Mataifa umekumbwa na wimbi la tuhuma za ufisadi wa kimaadili za maafisa wake wa kulinda amani katika baadhi ya nchi maskini zaidi ulimwenguni.

Mahasimu wawili wakuu Sudan Kusini

 

Mwaka 2013 Sudan Kusini ilikumbwa na mapigano makali baina ya wafuasi wa Rais Salva Kiir na makamu wake wa zamani, Riek Machar.

Hadi hivi sasa mamia ya wananchi wa Sudan Kusini wameshauawa na maelfu ya wengine wamekuwa wakimbizi.

Hii ni katika hali ambayo, siku chache zilizopita, Rais Salva Kiir wa Sudan Kusini alitamka bayana kwamba Marekani ndiyo inayosababisha ukosefu wa amani ndani ya nchi hiyo changa zaidi barani Afrika.

Rais Kiir aliyasema hayo katika mkutano wa viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) mjini Kampala Uganda na kuongeza kuwa, Marekani ndicho chanzo cha kurefuka mgogoro wa Sudan Kusini kutokana na nchi hiyo ya kibeberu kuiwekea masharti magumu serikali ya Juba sambamba na kuyapatia silaha makundi ya waasi yanayopiganana serikali yake.