Waturuki 2 wauawa, Mkenya ajeruhiwa katika shambulizi la kigaidi Mogadishu
Watu sita wakiwemo Waturuki wawili wameuawa katika shambulizi lililolenga basi dogo lililokuwa limebeba wafanyakazi wa hospitali moja inayosimamiwa na Uturuki katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Ripoti zinasema watu waliokuwa na silaha walilifyatulia risasi gari hilo katika wilaya ya Hodan mjini Mogadishu na kuua watu sita wanne miongoni mwao wakiwa raia wa Somalia na raia wawili wa Uturuki. Ripoti nyingine zinasema basi hilo dogo lilikuwa na wanafunzi wa raia wa Uturuki wanaoishi nchini Somalia na kwamba Muazerbaijan mmoja ni kati ya waliouliwa katika hujuma hiyo.
Raia wengine 6 wa Uturuki na Mkenya mmoja wamejeruhiwa katika mashambulizi hilo la kigaidi.
Hadi tunaandika habari hii hakuna kundi lililokuwa limedai kuhusika na shambulio hilo.
Wapiganaji wa kundi la kigaidi la al Shabab wamekuwa wakifanya mashambulizi kama hayo katika maeneo mbalimbali ya Somalia hususan vituo na hotoleli zinazotumiwa na wageni katika mji mkuu wa nchi hiyo Mogadishu.