Homa ya uti wa mgongo yaendelea kuaw watu Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i41391-homa_ya_uti_wa_mgongo_yaendelea_kuaw_watu_sudan_kusini
Afisa mmoja wa masuala ya kiutaalamu wa Shirika la Afya Duniani WHO ameripoti habari ya kupoteza maisha karibu watu 30 kutokana na homa ya uti wa mgongo nchini Sudan Kusini.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Mar 09, 2018 00:20 UTC
  • Homa ya uti wa mgongo yaendelea kuaw watu Sudan Kusini

Afisa mmoja wa masuala ya kiutaalamu wa Shirika la Afya Duniani WHO ameripoti habari ya kupoteza maisha karibu watu 30 kutokana na homa ya uti wa mgongo nchini Sudan Kusini.

Ramadhan Otim ametoa ripoti hiyo na kuongeza kuwa, kuenea homa ya uti wa mgongo huko kusini mashariki mwa Sudan Kusini kumeshasababisha vifo vya watu 28 hadi hivi sasa.

Amesema, watu 107 wameambukiwa ugonjwa huo hivi karibuni huko Sudan Kusini na hivi sasa wako chini ya uangalizi wa madaktari.

 

Mtaalamu huyo wa Shirika la Afya Duniani ametahadharisha kuwa, iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa katika maeneo yaliyokumbwa na ugonjwa huo katika jimbo la Imatong, la kusini mashariki mwa Sudan Kusini, basi kuna hatari ya kuenea zaidi ugonjwa huo na kuua watu wengi zaidi.

Homa ya uti wa mgongo ni tishio kwa Sudan Kusini kama ilivyo tishio kwa nchi nyingine 26 za Afrika.

Maambukizi ya homa hiyo hatari yalianza kushuhudiwa Sudan Kusini mwezi Mei, 2013.