Umoja wa Mataifa waongeza muda wa oparesheni zake za amani Sudan Kusini
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i41723-umoja_wa_mataifa_waongeza_muda_wa_oparesheni_zake_za_amani_sudan_kusini
Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha uamuzi wa kuongezea muda Oparesheni Maalumu ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) hadi tarehe 15, Machi mwaka 2019.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 16, 2018 03:24 UTC
  • Umoja wa Mataifa waongeza muda wa oparesheni zake za amani Sudan Kusini

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha uamuzi wa kuongezea muda Oparesheni Maalumu ya Kulinda Amani ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini (UNMISS) hadi tarehe 15, Machi mwaka 2019.

Uamuzi huo umezitaka pande mbalimbali za Sudan Kusini zisimamishe vita mara moja, na kusema Baraza la Usalama litafikiria kuchukua hatua zinazowezekana kuwaadhibu watu wanaovuruga amani, utulivu na usalama wa Sudan Kusini.

Kikao hicho pia kimeamua kudumisha ukubwa wa oparesheni hiyo iliyo na askari wasiozidi elfu 17 na polisi 2,101. Askari hao watakuwa ni pamoja na wale wa kikosi cha ulinzi cha kikanda kitakachoundwa chini ya idhini ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, lakini hakitakuwa na askazi zaidi ya elfu 4.

Mahasimu wakuu Sudan Kusini Rais Salva Kiir (kushoto) na kiongozi wa waasi Riek Machar

Vita vya ndani nchini humo vilivyoanza Disemba 2013 vimesababisha mauaji ya maelfu ya watu na kulazimisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi. Nchi hiyo ilitumbukia katika vita vya ndani baada ya Rais Salva Kiir kutoka kabila la Dinka kumtuhumu makamu wake wa zamani, Riek Machar wa kabila la Nuer kwamba alihusika na jaribio la kupindua serikali yake.