Joseph Mbilinyi (Sugu): Kuna maana gani Tanzania kufungua ubalozi wake Israel na kuwaacha Wapalestina
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i44912-joseph_mbilinyi_(sugu)_kuna_maana_gani_tanzania_kufungua_ubalozi_wake_israel_na_kuwaacha_wapalestina
Mbunge wa Mbeya mjini wa chama cha upinzani nchini Tanzania (CHADEMA) Joseph Osmund Mbilinyi maarifa kwa jina la Sugu amesema kuwa, inashangaza kuona hii leo serikali ya Rais John Magufuli inakwenda kinyume na misingi iliyojengwa na Tanzania katika kuwatetea watu wanaokandamizwa duniani, hususan Palestina.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 24, 2018 07:47 UTC
  • Joseph Mbilinyi (Sugu): Kuna maana gani Tanzania kufungua ubalozi wake Israel na kuwaacha Wapalestina

Mbunge wa Mbeya mjini wa chama cha upinzani nchini Tanzania (CHADEMA) Joseph Osmund Mbilinyi maarifa kwa jina la Sugu amesema kuwa, inashangaza kuona hii leo serikali ya Rais John Magufuli inakwenda kinyume na misingi iliyojengwa na Tanzania katika kuwatetea watu wanaokandamizwa duniani, hususan Palestina.

Akitoa mfano wa suala hilo mheshimiwa Mbilinyi ameelezea namna ambavyo Tanzania na kwa miaka mingi ilisimama kuwatetea watu wa nchi za Afrika Kusini, Msumbiji na kwengineko bila kusahau taifa madhlumu la Palestina. Amesema: "Mwalimu Nyerere alifuta uhusiano wa kibalozi na utawala wa Israel ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Wapalestina za kudai uhuru wao.

Raia madhlumu wa Palestina wanaoendelea kuuliwa shahidi kila siku na utawala katili wa Israel

Sasa tujiulize, hii leo Tanzania inaenda kufungua ubalozi Israel je ile stratijia ya Mwalimu Nyerere ya kuwaunga mkono Wapalestina imefikia wapi? Kwa sababu hali imezidi kuwa mbaya kwa sababu hivi sasa Wapalestina wa maeneo ya Ukanda wa Gaza na maeneo mengine yanayokaliwa kwa mabavu wanazidi kuuawa." Amesema mbunge wa Mbeya mjini.

Augustine Mahiga, Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania anayelaumiwa kwa kuiunga mkono Israel na kuwasahau Wapalestina wanaodhulumiwa

Aidha mbunge huyo wa chama kikuu cha upinzani ameonyesha kushangazwa na hatua ya Tanzania ya kufungua mahusiano na nchi ya Morocco na kuwasahau wakazi wa eneo la Sahara Magharibi chini ya harakati ya Polisario kutokana tu na ahadi ya kujengewa uwanja wa mpira iliyotolewa na serikali ya Rabat kwa Tanzania, chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli. Kwa mujibu wa mbunge huyo wa Mbeya mjini, amesema kuwa hata huyo Nyerere aliko anashangazwa na mambo yanavyoendeshwa hivi sasa nchini.