Algeria yalaani jinai za Israel huko Palestina na uungaji mkono wa Marekani
Waziri Mkuu wa Algeria amesema Algiers inapinga vikali jinai na mauaji yanayoendelea kufanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel huko Palestina licha ya uungaji mkono wa Marekani kwa utawala huo.
Ahmed Ouyahia ameashiria uiungaji mkono na misaada ya pande zote ya Marekani kwa utawala katili wa Israel na kusema: Inasikitisha kuona kwamba, watenda jinai hao dhidi ya raia wa Palestina wanapewa kinga ya kimataifa.
Waziri Mkuu wa Algeria amelaani vikali jinai zinazofanywa na Israel dhidi ya taifa la Palestina na kusema masuala ya kimataifa sawa yawe na karibu au mbali yana madhara kwa Algeria na kwamba nchi hiyo inalipa gharama za kushikamana na misimamo yake imara.
Ahmed Ouyahia amesisitiza kuwa Algeria itaendelea kusimama kidete dhidi ya ugaidi wa aina zote,