Mnangagwa: Nilikuwa karibu sana na mlipuko; uchaguzi utaendelea kama ilivyopangwa + Video
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i46264-mnangagwa_nilikuwa_karibu_sana_na_mlipuko_uchaguzi_utaendelea_kama_ilivyopangwa_video
Rais wa Zimbabwe amesema kuwa uchaguzi wa rais nchini humo utafanyika tarehe 30 Julai kama ilivyopangwa licha ya kile kinachosemekana ni jaribio la kutaka kumua jana Jumamosi.
(last modified 2026-01-14T11:42:18+00:00 )
Jun 24, 2018 13:16 UTC

Rais wa Zimbabwe amesema kuwa uchaguzi wa rais nchini humo utafanyika tarehe 30 Julai kama ilivyopangwa licha ya kile kinachosemekana ni jaribio la kutaka kumua jana Jumamosi.

Emmerson Mnangagwa ameyasema hayo baada ya mlipuko wa jana uliolenga mkutano wa kampeni za uchaguzi katika mji wa Bulawayo ambako makumi ya watu walijeruhiwa, wakiwemo maafisa kadhaa wa serikali.   

Maafisa nchini Zimbabwe wameeleza kuwa mipango ya usalama itaangaliwa upya. Uchaguzi huu ni wa kwanza tangu kupinduliwa madarakani Robert Mugabe huku Mnangagwa akiahidi kuwa utafanyika kwa amani na utulivu. Kwa upande wake kiongozi wa upinzani Nelson Chamisa amelaani mlipuko huo na kusema kuwa machafuko yoyote ya kisiasa hajakubaliki kivyovyote vile. 

Makamu wawili wa Rais wa Zimbabwe, ni miongoni mwa shakhsia waliojeruhiwa kwenye mlipuko huo wa jana huko Bulawayo.