Watoto wawili wauawa kwa mripuko wa bomu nchini Algeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i47547-watoto_wawili_wauawa_kwa_mripuko_wa_bomu_nchini_algeria
Mripuko wa bomu moja lililotengenezwa kienyeji umepelekea watoto wadogo wawili kuuawa na kujeruhiwa watu wengine wanne nchini Algeria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 19, 2018 10:21 UTC
  • Watoto wawili wauawa kwa mripuko wa bomu nchini Algeria

Mripuko wa bomu moja lililotengenezwa kienyeji umepelekea watoto wadogo wawili kuuawa na kujeruhiwa watu wengine wanne nchini Algeria.

Mtandao wa habari wa al Yaum al Saabii umeinukuu idara kuu ya ulinzi ya mji wa Bouïra, makao makuu ya mkoa wa Bouïra wa kaskazini mwa Algeria ikitangaza habari hiyo na kusema kuwa, bomu hilo limeripuka katika kitongoji kimoja cha mkoa huo.

Idara hiyo imeongeza kuwa, bomu hilo lilikuwa limetegwa na kundi moja la magaidi na hivi sasa jeshi la Algeria linaendesha msako wa kuwatafuta magaidi hao.

Licha ya serikali ya Algeria kuchukua hatua mbalimbali za kupambana na magenge ya kigaidi na kuimarisha ulinzi katika maeneo ya mpakani, lakini mara kwa mara huwa kunaripotiwa matukio kama hayo yakiwemo ya miripuko ya mabomu yanayotengenezwa kienyeji ambayo mara nyingi huwalenga maafisa wa jeshi.