Kamanda Azali Assoumani achaguliwa kuwa Rais wa Comoro
(last modified Fri, 15 Apr 2016 16:47:02 GMT )
Apr 15, 2016 16:47 UTC
  • Kamanda Azali Assoumani achaguliwa kuwa Rais wa Comoro

Kamanda Azali Assoumani, aliyewahi kufanya mapinduzi ya kijeshi nchini Comoro, amechaguliwa kuwa rais wa visiwa hivyo.

Kwa mujibu wa matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa leo Ijumaa na Tume ya Uchaguzi ya Comoro, Assoumani ndiye mshindi wa duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini humo. Duru ya pili ya uchaguzi wa rais nchini Comoro ilifanyika siku ya Jumapili iliyopita.

Kamanda Azali Assoumani, anayeungwa mkono na Ahmed Abdallah Mohamed Sambi, rais wa zamani wa nchi hiyo ametangazwa kuwa mshindi kwa kupata asilimia 40.98 ya kura na hivyo kumshinda mpinzani wake Mohamed Ali Soilihi mgombea wa chama tawala aliyepata asilimia 39.87 ya kura.

Azali Assoumani alikuwa rais wa Comoro kuanzia mwaka 1999 hadi mwaka 2002 na kuanzia 2002 hadi 2006.