Mar 10, 2019 07:24 UTC
  • Jeshi la Niger laua magaidi 38 wa Boko Haram katika mapigano makali

Wizara ya Ulinzi wa Niger imetangaza kuwa, jeshi la nchi hiyo limewaangamiza magaidi 38 wa kundi la Boko Haram katika mapigano makali yaliyojiri kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa zinasema wanajeshi saba wa serikali waliuawa katika mapigano hayo yaliyojiri Ijumaa katika eneo hilo la kusini mashariki mwa Niger.

Imearifiwa kuwa magaidi hao wakufurishaji wa Boko Haram walikuwa na idadi kubwa ya silaha wakati waliposhambulia kituo cha kijeshi karibu na Gueskerou katika eneo la Diffa.

Boko Haram ni kundi lenye misimamo ya kufurutu mipaka ambalo chimbuko lake ni kaskazini mwa Nigeria. Kundi hilo la magaidi lina ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, na limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji sambamba na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo. Magaidi wa Boko Haram wameeneza ugaidi wao katika nchi jirani za Niger na Cameroon.

Magaidi wa Boko Haram

Utawala wa Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria umeshindwa kuwaangamiza magaidi hao huku baadhi ya majenerali jeshini wakituhumiwa kuwa wanafaidika na kuendelea vitendo vya kigaidi nchini humo.

Tags