Jul 04, 2019 09:57 UTC
  • Vitendo vya ugaidi Tunisia, mada za miripuko zapatikana msikitini kabla ya kuripuka

Maafisa usalama wa Tunisia wamegundua mada kadhaa za miripuko katika msikiti mmoja nchini humo na kuzitegua kabla ya kuripuka.

Shirika la habari la Sputnik limeripoti habari hiyo na kuongeza kuwa, maafisa usalama wa Tunisia wamegundua miripuko mingi katika msikiti mmoja nje ya mji mkuu Tunis na kuitegua kabla haijaripuka na kusababisha maafa. Redio ya taifa ya Tunisia nayo imetangaza habari hiyo na kusema kuwa, miripuko hiyo ambayo ni mingi imegunduliwa kwenye masanduku kadhaa ndani ya msikiti huo.

Alkhamisi ya wiki iliyopita pia, Tunisia ilikumbwa na miripuko miwili ya kigaidi, mmoja ulilenga doria ya polisi katika barabara ya Charles de Gaulle na kuua afisa mmoja wa polisi na kujeruhi watu wengine watano wakiwemo polisi wawili na raia watatu. Mripuko wa pili ulitokea katika kitengo cha polisi cha kupambana na ugaidi cha eneo la al Farjan na kujeruhi watu wanne. Genge la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) limetangaza kuhusika na miripuko hiyo.

Hali tete ya kiusalama nchini Tunisia

 

Miripuko hiyo imetokea katika hali ambayo, mwezi Mei mwaka huu, serikali ya Tunisia iliwaweka tayari askari wake wa ulinzi waliotumwa katika mipaka ya kusini mashariki mwa nchi hiyo na Libya. Baadhi ya duru za kiitelijinsia zilitangaza kuwa Tunisia imepokea taarifa kutoka muungano wa kimataifa wa kupambana na genge la kigaidi la Daesh huko Iraq na Syria kwamba kiongozi wa kundi hilo Abubakar al Baghdadi yupo nchini Libya. Duru za habari za Tunisia zilitangaza kuwa al Baghdadi alikimbilia Libya kujificha baada ya wapiganaji wake kupata kipigo kikali katika eneo la Baghur nchini Syria.  

Tags