Malami: Mabilioni ya dola fedha za umma yameibwa nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i553-malami_mabilioni_ya_dola_fedha_za_umma_yameibwa_nchini_nigeria
Waziri wa Sheria wa Nigeria amesema kuwa mabilioni ya dola fedha za umma yameibwa nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 04, 2016 03:51 UTC
  • Malami: Mabilioni ya dola fedha za umma yameibwa nchini Nigeria

Waziri wa Sheria wa Nigeria amesema kuwa mabilioni ya dola fedha za umma yameibwa nchini humo.

Waziri wa Sheria wa Nigeria Abubakar Malami ametoa taarifa akisema kuwa, katika kipindi cha miaka 12 iliyopita zaidi ya dola bilioni elfu mbili ziliibwa kutoka katika hazina ya taifa. Malami amesema kuwa, utendaji mbaya katika mfumo wa fedha wa Nigeria, ombwe wa sheria katika mfumo wa vyombo vya mahakama na udhaifu wa taasisi za utekelezaji wa sheria ni miongoni mwa sababu za ufisadi na wizi wa mali ya umma nchini Nigeria.

Mwezi uliopita wa Januari serikali ya Nigeria ilitangaza kuwa, imewakamata maafisa wasiopungua 55 wa serikali iliyotangulia kwa tuhuma za kuhusika na ufisadi na ubadhirifu wa mali ya umma.