Njama mpya za serikali ya Nigeria dhidi ya Sheikh Zakzaky
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i55674-njama_mpya_za_serikali_ya_nigeria_dhidi_ya_sheikh_zakzaky
Serikali ya Nigeria imeanzisha njama mpya dhidi ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky na kudai kwamba eti anapanga njama za mapinduzi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 29, 2019 07:48 UTC
  • Njama mpya za serikali ya Nigeria dhidi ya Sheikh Zakzaky

Serikali ya Nigeria imeanzisha njama mpya dhidi ya Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky na kudai kwamba eti anapanga njama za mapinduzi.

Kwa mujibu wa matandao wa Intaneti wa African, serikali ya Nigeria imedai leo kuwa, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky amepokea msaada wa fedha kutoka Iran ili kufanya mapinduzi huko Nigeria.

Serikali ya Nigeria amefungua kesi katika Mahakama Kuu ya Shirikisho mjini Abuja na kudai kuwa wanachama wa Harakati ya Kiislamu hawaitambui serikali ya Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo.

Rais Muhammadu Buhari wa Nigeria ana uhusiano wa karibu sana na viongozi wa Saudi Arabia

 

Inasemekana kuwa serikali ya Nigeria imeanzisha njama mpya dhidi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky ili kummaliza kisiasa au kumpotezea maisha kabisa.

Mwezi uliopita, Harakati ya Kiislamu ya Nigeria ilitangaza kuwa, vibaraka na makachero wa serikali wanapanga njama za kumuua Sheikh Ibrahim Zakzaky wakati akiwa India kwa matibabu.

Tarehe 13 Disemba 2015, jeshi la Nigeria liliivamia Husainia ya Sheikh Ibrahim Zakzaky katika mji wa Zaria na kumpiga risasi mwanachuoni huyo pamoja na mkewe. 

Baada ya kuongezeka mashinikizo ya ndani na ya kimataifa, mwezi uliopita serikali ya Nigeria iliruhusu Sheikh Zakzaky aende India kwa matibabu lakini ilimuwekea vikwazo vingi vya kiusalama na kumpa madaktari wasioaminika, hivyo alilazimika kurudi Nigeria bila ya kufanyiwa matibabu yoyote.