Mkuu wa Harakati ya Kiislamu Nigeria kupelekwa jela kuu ya Kaduna
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i57709-mkuu_wa_harakati_ya_kiislamu_nigeria_kupelekwa_jela_kuu_ya_kaduna
Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna nchini Nigeria imekubali ombi la gavana wa jimbo hilo la kupelekwa Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe katika jela kuu ya jimbo hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 06, 2019 04:02 UTC
  • Mkuu wa Harakati ya Kiislamu Nigeria kupelekwa jela kuu ya Kaduna

Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna nchini Nigeria imekubali ombi la gavana wa jimbo hilo la kupelekwa Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria, Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe katika jela kuu ya jimbo hilo.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Mehr, Mahakama Kuu ya jimbo la Kaduna la Nigeria imechukua uamuzi usiotarajiwa wa kukubali kupelekwa kwenye jela kuu ya jimbo hilo Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe baada ya kuombwa kufanya hivyo na gavana wa Kaduna.

Hivi sasa Mkuu huyo wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria anashikiliwa sehemu isiyojulikana na kwa mujibu wa taarifa za uhakika, Sheikh Zakzaky anasumbuliwa na matatizo mengi ya kiafya.

Mahakama Kuu ya Kadunia hata haikugusia japo kwa mbali suala la hali ya kiafya ya sheikh huyo mwanaharakati.

Maandamano ya kutaka kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky nchini Nigeria

 

Mwezi Agosti mwaka huu, Sheikh Ibrahim Zakzaky alipelekwa India kwa matibabu lakini maafisa usalama wa serikali ya Nigeria walimuwekea vizuizi vingi na walimtishia hata kumuua, hivyo alilazimika kurejea Nigeria bila ya kufanyiwa matibabu yoyote.

Vikosi vya usalama vya Nigeria vilimchukua Sheikh Zakzaky na mkewe mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa mji mkuu Abuja na kumpeleka kusikojulikana.

Tarehe 13 Disemba 2015, jeshi la Nigeria lilifanya mauaji ya kikatili dhidi ya Waislamu wa Nigeria baada ya kuivamia Husainia ya mji wa Zaria na kumteka nyara Sheikh Zakzaky baada ya kumpiga risasi kadhaa.