Sheikh Zakzkay: Muqawama umezaliwa upya nchini Lebanon
Feb 24, 2025 03:06 UTC
Kiongozi wa Waislamu wa madhebeu ya Shia nchini Nigeria amesisitiza kuwa, kushiriki mamilioni ya watu katika mazishi ya Mashahidi wa Muqawama ni sawa na "kuzaliwa upya Muqawama wa Lebanon".
Sheikh Ibrahim Zakzaky, ambaye yuko Beirut alikokwenda kuhudhuria mazishi ya Mashahidi Sayyid Hassan Nasrullah na Sayyid Hashim Safiyyuddin, amesema katika mahojiano maalumu aliyofanyiwa hapo jana na mwandishi wa Shirika la Habari la Mehr aliyetumwa huko Lebanon kwamba kuhudhuria mamilioni ya watu katika mazishi ya makamanda wa Muqawama kunadhihirisha kuwa Muqawama umezaliwa upya nchini Lebanon.
Sheikh Zakzaky amesema: "Sayyid Hassan Nasrullah alikuwa nembo ya umma wa Kiislamu, na picha na matukio tuliyoyaona leo yameonyesha kuwa roho yake ingali iko kwenye medani. Maadui Wazayuni walidhani kwamba kwa kumuua yeye wataumaliza Muqawama, lakini matukio ya leo yamedhihirisha kuzaliwa upya kwa Muqawama wa Lebanon, na inshaaLlah mwisho wa harakati hii utakuwa ni kupatikana ushindi".../
Tags