Algeria: Kuitetea na kuiunga mkono Palestina ni katika sera zetu za nje
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63012-algeria_kuitetea_na_kuiunga_mkono_palestina_ni_katika_sera_zetu_za_nje
Msemaji wa serikali ya Algeria amesema kusimama na wananchi wa Palestina, kuwatetea na kuwaunga mkono nio katika sera za nje zilizopewa kipaumbele na taifa hilo la Kiarabu la kaskazini mwa Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 24, 2020 23:01 UTC
  • Algeria: Kuitetea na kuiunga mkono Palestina ni katika sera zetu za nje

Msemaji wa serikali ya Algeria amesema kusimama na wananchi wa Palestina, kuwatetea na kuwaunga mkono nio katika sera za nje zilizopewa kipaumbele na taifa hilo la Kiarabu la kaskazini mwa Afrika.

Ammar Belheimer amesema hayo katika mahojiano na shirika la habari la Sputnik na kueleza bayana kuwa, "wananchi wa Algeria na serikali inawaunga mkono Wapalestina."

Amesema serikali ya Algeria inaunga mkono maslahi ya Wapalestina, mamlaka yao ya kujitawala na haki zao. Msemaji wa serikali ya Algiers ameongeza kuwa, nchi hiyo itaendelea kuwapa himaya Wapalestina na kuunga mkono kadhia ya Palestina.

Haya yanajiri siku chache baada ya Jumuiya ya Maulamaa wa Algeria kusema kuwa, ni haramu kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala ghasibu wa Kizayuni wa Israel.

Maandamano ya kupinga usaliti huo wa Imarati yanaendelea kushuhudia katika kona mbalimbali za dunia

Taarifa ya jumuiya hiyo ambayo ni kubwa zaidi ya maulamaa wa nchi hiyo imesisitiza kuwa, kushirikiana na kuanzisha uhusiano wa kawaida na utawala huo ghasibu na vamizi ambao umeighusubu ardhi ya Palestina na kukanyaga matukufu yake ukiwemo msikiti wa Al Aqsa pamoja na watu wake ni uhaini na usaliti mkubwa ambao hauwezi kunyamaziwa.

Baadhi ya vyama vya siasa nchini Algeria, navyo pia vimelaani vikali makubaliano yaliyofikiwa kati ya Imarati na utawala wa Kizayuni na kuyaelezea makubaliano hayo kuwa ni sawa kuwasaliti na kuwachoma jambia kwa nyuma wananchi wa Palestina.