Rais Uhuru ahutubia taifa huku akiahidi mustakbali mwema wa nchi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64585-rais_uhuru_ahutubia_taifa_huku_akiahidi_mustakbali_mwema_wa_nchi
Rais Uhuru Kenya wa Kenya leo Alhamisi amehutubia taifa kwa mara ya saba bungeni jijini Nairobi akiwaambia Wakenya kwamba taifa hilo lingali lina nguvu, jasiri na lenye matarajio ya mustakbali mwema.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 12, 2020 10:57 UTC
  • Rais Uhuru ahutubia taifa huku akiahidi mustakbali mwema wa nchi

Rais Uhuru Kenya wa Kenya leo Alhamisi amehutubia taifa kwa mara ya saba bungeni jijini Nairobi akiwaambia Wakenya kwamba taifa hilo lingali lina nguvu, jasiri na lenye matarajio ya mustakbali mwema.

Katika hotuba yake hiyo ya saba kwa taifa, Rais Uhuru Kenyatta ameashiria namna Kenya ilivyokumbwa na maambukizi ya corona na kukiri kuvurugika uchumi, sekta za jamii na afya duniani vilivyomzuia kushindwa kuhutubia taifa kwa muda wa miezi sita.

Hotuba hiyo ilipasa kutolewa na Rais Kenyatta katika robo ya kwanza ya mwaka huu hata hivyo ilisitishwa kutokana na maambukizi ya virusi vya corona huko Kenya. Rais Uhuru Kenyatta kwa mara ya mwisho alihutubia taifa tarehe 4 Aprili mwaka 2019. Kuhusu janga la corona, Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema katika hotuba yake hiyo ya leo kwamba, licha ya kutekelezwa juhudi zinazofaa za kudhibti maambukizi ya Covid-19 nchini humo lakini maambukizi ya corona yangali yanaongezeka na yamesababisha wasiwasi kwa taifa.

Hadi kufikia leo, jumla ya watu 66,723 wameambukizwa corona nchini Kenya huku 1,203 wakiripotiwa kuaga dunia. Rais Kenyata aidha amewapongeza matabibu na wafanyakazi wa huduma za afya kwa kazi yao kubwa katika kipindi hiki cha kukabiliana na maambukizi ya corona.

Kenya katika mapambano dhidi ya corona 

Katika sehemu nyingine ya hotuba yake, Rais wa Kenya amewahakikishia Wakenya kwamba, wanafunzi ambao bado wako nyumbani wataanza tena masomo mwezi Januari mwakani kutokana na vizuizi vya corona. Amesema; utaratibu wa kufungua shule polepole na kwa awamu unafuatiliwa hivi sasa katika ngazi zote ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi. Vilevile Rais wa Kenya ametangaza ajira laki moja kwa vijana.