Zimbabwe yaanza tena kutekeleza karantini nchi nzima
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i65557-zimbabwe_yaanza_tena_kutekeleza_karantini_nchi_nzima
Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa sheria ya karantini ya nchi nzuma imeanza kutekelezwa nchini humo kwa mara nyingine tena kuanza jana usiku kutokana na kuongezeka maambukizi mapya ya corona.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 03, 2021 04:29 UTC
  • Zimbabwe yaanza tena kutekeleza karantini nchi nzima

Serikali ya Zimbabwe imetangaza kuwa sheria ya karantini ya nchi nzuma imeanza kutekelezwa nchini humo kwa mara nyingine tena kuanza jana usiku kutokana na kuongezeka maambukizi mapya ya corona.

Waziri wa Afya na Makamu wa Rais wa Zimbabwe amesisitiza kuwa, nchi hiyo imeanza mara moja kutekeleza sheria kali ya karantini ya nchi nzima kwa kuzingatia kuongezeka hivi karibuni maambukizi mapya ya ugonjwa wa Covid-19 nchini humo. 

Takwimu rasmi za karibuni zilizotangazwa na Wizara ya Afya ya Zimbabwe zinaonyesha kuwa,  tangu kuenea maambukizi ya corona huko Zimbabwe had sasa watu elfu 14 na 84 wameripotiwa kuugua ugonjwa wa Covid-19 nchini humo; huku wengine 369 wakiaga dunia mwa ugonjwa huo. 

Zimbabwe yaanza tena kutekeleza sheria ya karantini  

Nchi hiyo ya kusini mwa bara la Afrika mwanzoni mwa miaka ya elfu mbili ilikumbwa na mgogoro mkubwa wa kiuchumi na ambao ulisababisha kusambaratisha mfumo wa afya ya umma nchini humo.  

Kwa mara ya kwanza mwezi Machi mwaka jana Zimbabwe ilikuwa chini ya karantini ya nchi nzima;  na kuanzia mwezi Mei  ilianza kupunguza kwa kiasi kikubwa vizuizi vya karantini kwa nchi nzima.