Waalgeria watatu watiwa mbaroni kwa tuhuma za ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i6586-waalgeria_watatu_watiwa_mbaroni_kwa_tuhuma_za_ugaidi
Jeshi la Algeria limewatia mbaroni raia watatu wa nchi hiyo kwa tuhuma za kuyasaidia makundi ya kigaidi nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 07, 2016 11:38 UTC
  • Waalgeria watatu watiwa mbaroni kwa tuhuma za ugaidi

Jeshi la Algeria limewatia mbaroni raia watatu wa nchi hiyo kwa tuhuma za kuyasaidia makundi ya kigaidi nchini humo.

Shirika la habari la serikali ya Qatar (QNA) limeripoti habari hiyo kutoka mjini Algiers, Algeria na kuongeza kuwa, Wizara ya Ulinzi ya nchi hiyo leo Jumamosi imetangaza kwamba, wanajeshi wa nchi hiyo wamewatia mbaroni watu watatu kwa tuhuma za kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi baada ya kuwafuatilia kwa muda.

Taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Algeria imeongeza kuwa, katika kupambana na magaidi, jeshi la nchi hiyo limewatia mbaroni raia watatu wa Algeria kwa tuhuma za kushirikiana na magenge ya kigaidi katika maeneo ya Boumerdès kaskazini mwa Algeria na Bordj Bou Arréridj, mashariki mwa nchi hiyo ya kaskazini mwa Afrika.

Wizara ya Ulinzi ya Algeria imeongeza kuwa, jeshi la nchi hiyo limefanikiwa pia kuvunja maficho ya magaidi katika eneo la Baskikdah (?), kaskazini mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, wakati askari wa serikali ya Algeria walipoingia kwenye maficho hayo walikamata silaha kadhaa za magaidi hao.