Wasudani waandamana mbele ya ikulu ya rais wakilalamikia hali mbaya ya kiuchumi
(last modified Mon, 12 Apr 2021 10:29:48 GMT )
Apr 12, 2021 10:29 UTC
  • Wasudani waandamana mbele ya ikulu ya rais wakilalamikia hali mbaya ya kiuchumi

Wananchi wa Sudan wamefanya maandamano mbele ya ikulu ya rais wa nchi hiyo mjini Khartoum wakilalamikia hali mbaya ya uchumi na ughali wa maisha.

Maandamano hayo yamekabiliwa kwa mkono wa chuma na askari usalama ambao wametumia gesi ya kutoa macho kuzima harakati hiyo.

Maandamano hayo yamefanyika kwa mnasaba wa kutimiia mwaka wa pili tangu wananchi wa Sudan walipoindoa madarakani serikali ya kiongozi wa zamani wa nchi hiyo, Omar al Bashir.

Maandamano hayo yanafanyika baada ya takwimu kuonyesha kuwa kiwango cha mfumuko wa bei nchini Sudan umefikia asilimia 400 huku bei za bidhaa zikiongezeka mara 20. 

Wasudani wakipinga hali mbaya ya kiuchumi

Wananchi wa Sudan wanaamini kuwa hali mbaya ya kiuchumi ya nchi hiyo hivi sasa ni mbaya sana ikilinganishwa na wakati wa utawala wa Omar Hassan al Bashir kutokana na kupungua mtawalia thamani ya sarafu ya nchi hiyo, na uhaba wa bidhaa muhimu za kila siku kama mafuta ya petroli, mkate na dawa. 

Sudan ilianza kushuhudia wimbi la maandamano ya wananchi tarehe 19 Disemba mwaka 2018 dhidi ya hali mbaya ya uchumi na kufuatia ghasia hizo jeshi la Sudan tarehe 11 Aprili mwaka jana lilimuondoa madarakani rais huyo wa zamani na kushika hatamu za uongozi kwa kuunda baraza la kijeshi, ambalo nalo baadaye lilivunjwa baada ya kuundwa serikali ya mpito. 

Tags