Makumi wa wanachama wa Boko Harama waangamizwa na jeshi la Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i71948-makumi_wa_wanachama_wa_boko_harama_waangamizwa_na_jeshi_la_nigeria
Jeshi la Nigeria limetangaza habari ya kuangamiza makumi ya magaidi wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 03, 2021 08:09 UTC
  • Makumi wa wanachama wa Boko Harama waangamizwa na jeshi la Nigeria

Jeshi la Nigeria limetangaza habari ya kuangamiza makumi ya magaidi wa kundi la kigaidi la Boko Haram katika jimbo la Borno, kaskazini mashariki mwa nchi.

Jenerali Benard Onyeuko, Mkurugenzi wa Habari wa Jeshi la Nigeria, amesema magaidi wasiopungua 73 wa Boko Haram wameuawa katika operesheni ya maafisa usalama dhidi ya kundi hilo katika miji tofauti ya jimbo la Borno baina ya Juni 18-30.

Amesema mbali na magaidi 73 kungamizwa wakati wa operesheni hiyo, lakini pia vyombo vya usalama vimefanikiwa kukamata idadi kubwa ya silaha, magari na risasi zilizokuwa zikitumiwa na magaidi hao.

Jenerali Onyeuko ameongeza kuwa watu 55, wakiwemo watoto 27, ambao walikuwa wanashikiliwa mateka na magaidi hao, waliokolewa wakati wa operesheni hizo.

Wanajeshi wa Nigeria katika operesheni dhidi ya Boko Haram

Tokea mwaka 2009 hadi sasa, Nigeria imo vitani kupambana na magaidi wa Boko Haram ambao wametangaza utiifu wao kwa genge la kigaidi la Daesh (ISIS). 

Mgogoro wa Boko Haram umeshaua watu wasiopungua 36,000 na kusababisha mamilioni ya wengine kuwa wakimbizi ndani na nje ya Nigeria hasa katika maeneo yanayopakana na Ziwa Chad.