Nigeria: Watu wenye silaha wameteka nyara wanafunzi 140 katika jimbo la Kaduna
Kundi moja la wanamgambo wenye silaha limewateka nyara wanafunzi 140 katika shambulio lililofanya katika shule moja ya sekondari katika jimbo la Kaduna, huko kaskazini magharibi mwa Nigeria usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita.
Watu waliokuwa na silaha wamewateka nyara wanafunzi hao 140 kwa ajili ya kuwatumia kama chambo ya kupatiwa mlungura.
Emmanuel Paul, mwalimu anayefundisha katika shule ya sekondari ya bweni ya Bethel jimboni Kaduna amesema kuwa, wahalifu hao wamewateka nyara wanafunzi 140 na kwamba wanafunzi wengine 25 walifanikiwa kukimbia. Amesema, wanafunzi wasiopungua 165 walikuwa wamelala wakati wa shambulio hilo.
Hilo ni shambulio la tatu kubwa kutokea katika jimbo la Kaduna katika siku za hivi karibuni.
Hadi sasa hakuna kundi lolote liilotangaza kuhusika na hujuma ya sasa iliyopelekea kutekwa ntaya wafunzi 140. Hata hivyo wiki kadhaa iliopita kundi la kigaidi na kitakfiri wa Boko Haram liliteka nyara wanafunzi zaidi ya 300 katika jimbo la Katsina.
Jumapili iliyopita, wafanyakazi wasiopungua wanane wa hospitali ya Kaduna walitekwa nyara na watu wasiojulikana.
Samuel Aruwan Kamishna wa Usalama wa Ndani katika jimbo la Kaduna amesema kuwa, watu waliokwa na silaha waliwauwa watu wengine saba jimboni humo.
Jimbo la Kaduna huko kaskazini magharibi mwa Nigeria limekuwa likikabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara watu wenye silaha.